Nembo ya chama cha soka Dar es salaam na klabu ya Besiktas
Kasongo ameyasema hayo leo wakati wa kumuaga Rabbin Sanga ambaye anakwenda kufanya majaribio ya siku 10 katika klabu hiyo ya ligi kuu ya Uturuki ambayo pia inashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nyingi.
''Haikuwa rahisi kabisa lakini sasa tumefanikiwa kuandaa mtaala mzuri kwaajili ya soka la vijana na tunajipanga kuwa na mashindano bora ya vijana ambayo yatazalishwa vipaji vingi kama Rabbin Sanga'', amesema Kasongo.

Rabbin mwenye fulana nyeusi karibu na Kinasa sauti cha EATV. Hapo ni wakati akifanyiwa dua ya kuagwa leo.
Kwa upande wake Rabbin amesema, amejiandaa vya kutosha akitoa pongezi za pekee kwa kocha wake katika timu ya vijana ya Bombom United, Amri Bonge kwa kusema amemwandaa vizuri na anaamini atafanya vizuri katika majaribio hayo.
Sanga atakwenda kwenye kikosi cha Besiktas cha vijana chini ya umri wa miaka 16 ambapo atafanya majaribio na kama atafuzu atasajiliwa moja kwa moja.






