Jumanne , 6th Nov , 2018

Aliyekuwa mke halali wa mchekeshaji na muigizaji  Mkono Mkonole ameibuka na kuiambia eNEWZ kwamba mume wake huyo ametoroka nyumbani na kumuachia barua kitandani.

Msanii Mkono wa mkonole

Mke huyo wa Mkono aitwaye Sabrina Ally, amesema baada ya madeni kuwa mengi na kuwazidia yeye na mume wake, ndipo alipoamua kutoroka na kukimbia majukumu huku akiacha barua kitandani ikiwa na maagizo ya kujitosheleza.

Sabrina anasema barua hiyo ilikuwa ina ujumbe ufuatao "Sabrina mke wangu mimi mumeo Fadhili naandika barua hii kwa akili zangu timamu, mimi nimeamua kuondoka kutokana na maisha magumu ambayo tumekuwa tukiyaishi tangu tumeoana nimeamua kuondoka kwenda Kyela kwa mjomba kutafuta maisha na nikipata nitarudi ila sijakuacha mke wangu"aliandika hivyo Mkono.

Sabrina anamalizia kwa kuongea kwamba Mkono alivyoondoka aliacha madeni mengi ikiwepo deni la Benki ambalo liliwekewa dhamana ya hati ya nyumba ya baba yake hivyo pamoja na kwamba Mkono kashaanzisha maisha mengine  anaomba aje alipe deni la watu alilokuwa anadaiwa ili kuzuia nyumba ya baba yake isiuzwe.