Jumanne , 3rd Jan , 2017

Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati ya Mchezo wa Judo yanatarajiwa kuanza tarehe 01 mpaka 03 Machi mwaka huu visiwani Zanzibar.

Judo

Akizungumza na Hotmix Michezo Katibu Mkuu wa Chama cha Judo nchini JATA Innocent Mallya amesema wapo katika maandalizi ya mwisho na wiki ijayo wanatarajia kutaja kikosi kitakachoshiriki katika mashindano hayo.

Wakati huohuo Mallya amesema, wamepata ofa kutoka Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ya kupeleka wachezaji watatu kambini nchini Hungary kwa ajili ya maandalizi ya Olimpiki 2020 yatakayofanyika jijini Tokyo nchini Japan.

Mallya amesema, mpaka sasa wameshapata wachezaji watatu ambao ni wa uzito wa juu, wa kati na wa chini ambao wataingia kambini kwa ajili ya maandalizi ambapo ameongeza kuwa nchi hiyo pia inaandaa Mashindano ya dunia yatakayofanyika Oktoba mwaka huu nchini humo hivyo wachezaji hao watapata pia nafasi ya kushiriki katika mashindano hayo.