
Jina halisi la Sir Mo Farah ni Hussein Abdi Kahin
"Watu wengi wananijua kama Mo Farah, lakini sio jina langu. Hadithi halisi ni kwamba nilizaliwa kaskazini mwa Somalia, kama Hussein Abdi Kahin. Licha ya kile nilichosema katika siku za nyuma, wazazi wangu hawakuwahi kuishi Uingereza. Nilipokuwa na umri wa miaka 4, Baba yangu aliuwawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe (Somalia). Nilitenganishwa na Mama yangu, na nililetwa Uingereza kinyume cha sheria chini ya jina la mtoto mwingine aitwaye Mohamed Farah." Amesema Mo Farah
Sir Mo Salah ni mwengereza wa kwanza kushinda Medali 4 za dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki amesema historia yake ya utotoni ndio iliyomsukuma kupata mafanikio hayo. Sir Mo pia ameshinda medali 6 za dhahabu kwenye michuano ya Dunia ya riadha.