Jumanne , 9th Jun , 2020

Mfanyabiashara na muwekezaji wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji "Mo", amewatoa wasiwasi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo, kwa kusema hakuna mchezaji yeyote atakayeondoka pia watamsajili mchezaji yeyote kutoka popote kama kocha wao akimuhitaji.

Mfanyabishara na Muwekezaji wa Klabu ya Simba Mohamed Dewji "Mo"

Akitangaza hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter muda mfupi uliopita Mo Dewji ameeleza kuwa

"Wanasimba wenzangu nataka niwahakikishie, hakuna mchezaji wetu yeyote atakayeondoka Simba lakini pia tutasajili mchezaji yeyote kutoka popote, kama Mwl wetu atamuhitaji kwenye kikosi chake, Tutashuka kwa kishindo hatuna maneno mengi lakini tupo" amendika Mo Dewji.