Jumatatu , 2nd Mar , 2020

Nyota ya staa wa Tanzania na mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa imeendelea kung'ara usiku wa jana, akiweka historia ya kucheza mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi 'Carabao Cup' dhidi ya Manchester City katika uwanja wa Wembley.

Mo Dewji na Mbwana Samatta

Mchezo huo ulimalizika kwa Aston Villa kupoteza kwa mabao mawili kwa moja, huku bao la Aston Villa likifungwa na Mbwana Samatta katika dakika ya 41 ya mchezo.

Malalamiko ya mashabiki wengi wa Tanzania hasa katika mtandao wa Twitter ni juu ya mchezaji huyo kutopewa alama ya blue 'Verification' kutoka kwa mtandao huo na miongoni mwao ni bilionea na mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo' ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter amemuomba mmoja wa wahusika wa masuala ya teknolojia katika mtandao huo kumpa 'Verification' Samatta kwakuwa ni mtu maarufu Tanzania.