Jumatatu , 7th Dec , 2015

kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa amezitaka klabu za soka hapa nchini kuruhusu wachezaji wao kwenda nje ya nchi kucheza soka la kulipwa endapo nafasi zitatokea ili kuwapa uzoefu wa mechi za kimataifa.

kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars kwenye picha ya pamoja kuelekea moja ya mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Hayo ameyasema siku chache baada ya kumalizika kwa mashindano ya Cecafa Senior Chalenji nchini Ethiopia na kushuhudiwa Uganda ikiendeleza ubabe wake kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati kwa kutwaa ubingwa huku timu za Tanzania zikiondoka patupu.

Mkwasa amebainisha kuwa maendeleo ya soka nchini Uganda yamebebwa na misingi mizuri kwa soka la vijana lakini pia klabu zimeruhusu nyota wake ambao wengi wanacheza barani ulaya na nchi nyingine ambazo zimeendelea kwenye soka.

Ameongeza kuwa timu ya Taifa nzuri inajengwa na wachezaji bora wenye uzoefu na ligi zenye ushindani na kupelekea kuwa na mchango mzuri wanapokutana na timu imara kama Algeria na nyinginezo barani Africa.