Jumatatu , 7th Nov , 2016

Mkenya Mary Keitany amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda mbio za Marathon za Jiji la New York mara tatu katika kipindi cha miaka 30.

Mary Keitany - Mwanariadha wa Kenya

 

Keitany mwenye umri wa miaka 34, alitumia muda wa saa mbili, dakika 24 na sekunde 26 na kuwa mwanamke wa kwanza kufanya hivyo tangu raia wa Norway Grete Waitz - aliyeshinda mbio hizo mara tano mtawalia.

Bingwa wa dunia kutoka Eritrea Ghirmay Ghebreslassie, (20), alimshinda Mkenya Lucas Rotich katika mbio za wanaume na kuwa mshindi wa Marathon ya New York mwenye umri mdogo zaidi.

Ghebreslassie, aliyemaliza katika nafasi ya nne katika London Marathon na Olimpiki Rio alitumia muda wa saa 2, dakika 7 na sekunde 51 na kuwanyima Wakenya ubingwa wa nne mtawalia katika Marathon kwa wanawake na wanaume