Ijumaa , 12th Jun , 2015

Mabondia Francis Miyeyusho na Mganda Mbaraka Seguye wanatarajiwa kupanda ulingoni hapo kesho katika pambano lisilo la Ubingwa Raundi nane uzito wa unyoya ambalo ni Featherweight kilo 58.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania TPBO Yassin Abdallah Ustaadh amesema,wameamua kumleta bondia Mganda ambaye ni namba moja ili kuleta changamoto kwa Miyeyusho.

Ustaadh amesema, katika mapambano ya kesho Mada Maugo atapanda ulingoni kupambana na Jackob Maganga kuwania Ubingwa wa UBO ukanda wa Afrika huku Kalama Nyilawila akipambana na Allybaba Ramadhani.