Mratibu wa mpambano huo Musa Kova amesema kuwa kutokana na hilo Pambano kati ya mabondia Francis Miyeyusho dhidi ya bondia bingwa wa ufilipino Ronald Pontillas utaziba pengo,ambapo Utakuwa Mpambano wa ubingwa wa dunia uzito wa bantam kilo 59
Kova amesema uamuzi huo umezingatia ubora wa mabondia wote hao na pia kutoa fursa kwa watanzania kupata burudani ya ngumi za kimataifa hasa ikizingatiwa bondia Miyeyusho mchezo huo utakuwa pambano lake la kwanza kupigana na bondia wa nje akichezea nyumbani tanzania kwani amekua akicheza mapambano yake nje zaidi anapokua na pambano na bondia wa nje
Pambano hilo litasimamiwa na PST ambao kupitia katibu mkuu wake Anthony Rutta amesema kila kitu kiko sawa na wao kusimamia pambano hilo ni kutokana na uzoefu wao hasa kwa mabondia wanaotoka nchini Uphilipino.
