Jumanne , 1st Apr , 2014

Bondia mtanzania Francis Miyeyusho chichi mawe, amesema yuko tayari kwa kushuka ulingoni aprili 5 mwaka huu, kupambana na bondia bingwa wa Ufilipino Ronald Pontillas katika pambano la kuwania ubingwa wa dunia uzito wa bantam kilo 59.

Miyeyusho ametoa kauli hiyo hii leo wakati akiongea na East Africa radio kufuatiwa taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa bondia huyo ameamua kukacha pambano hilo.

Miyeyusho amesema kuwa awali kulikua na mkanganyiko wa tarehe ya mpambano huo na pili kulikua na mvutano kati yake na mama yake ambaye alikua akipinga miyeyusho kucheza mpambano hilo kwa madai taarifa ameipata ghafla lakini baada ya mazungumzo kila kitu kimewekwa sawa na amewahakikishia mashabiki wake kuwa atashuka ulingoni siku hiyo

Pambano hilo litasimamiwa na PST ambapo katibu mkuu wake Antony Rutta amesema kila kitu kuhusiana na pambano hilo kimekamilika na wageni hao kutoka uphilipino wakitaraji kwasili kesho kutwa.