
Anayepigwa ni Tony Ferguson na aliyepiga ngumi hiyo ni Justin Gaethje
Pambano hilo limepigwa bila mshabiki kwenye uwanja wa VyStar Veterans Memorial huko Jacksonville, Florida.
Awali pambano hilo lilitakiwa kupigwa 18 April huko Brooklyn lakini likaahirishwa kutokana na Janga la Corona na kupangiwa tarehe ambayo ni usiku wa Mei 10, 2020.
Justin Gaethje mwenye miaka 31, amempiga Tony Ferguson mwenye miaka 36 na sasa ndio bingwa wa UFC Lightweight na atapigana na Khabib Nurmagomedov katika pambano ambalo litapangiwa tarehe baadaye mwaka huu.
Justin Gaethje baada ya kukabidhiwa mkanda wa UFC Lightweight
Marekani bado inaendelea na Lockdown kutokana na kuwa muhanga mkubwa wa janga la Corona ambapo Mei 7, 2020 Rais Donald Trump aliongoza maombi ya kitaifa pamoja na viongozi wa dini.