Ijumaa , 5th Mei , 2017

Mchezaji wa timu ya Ruvu Shooting FC, Abdulrahaman Mussa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzani Bara kwa mwezi wa Aprili kwa msimu wa 2016/2017 baada ya kumshinda Jafar Salum kutoka Mtibwa Sugar FC na Zahoro Pazi wa Mbeya City

Abdulrahaman akiwa na wachezaji wenzake wa Ruvu Shooting FC

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umesema ushindi huo umekuja baada ya timu yake kucheza michezo miwili ambayo Abdulrahaman alicheza dakika zote 180 na kufunga magoli manne kati ya matano yaliyofungwa na timu yake na hivyo kuifanya timu yake kushuka nafasi moja na kuwa ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hata hivyo, mchezaji huyo aliweza kuifungia timu yake 'Hat trick' katika mchezo wao dhidi ya Majimaji uliofanyika katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.

Kutokana na kushindi tuzo hiyo, Abdulrahaman atazawadiwa kitita cha pesa taslimu Milioni Moja kutoka kwa wadhamini wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.