Kushoto ni Juma Nyangi wa Alliance FC, na kulia ni Gadiel Michael wa Yanga
Msemaji wa Alliance FC, Jackson Luka, amesema kamati ya nidhamu ya klabu hiyo ilimuita jana Machi 4, 2019, mchezaji huyo na kumhoji hivyo leo inaketi kwaajili ya kutoa maamuzi.
''Tulimsikiliza vizuri jana tena tulikuwa tuna tazama video ya tukio hilo alilofanya kwahiyo ametoa utetezi wake na kamati leo itatoa maamuzi yake lakini atarajie kupata adhabu kali'', amesema.

Juma Nyangi aliponaswa na Kamera za Azam TV akimshika makalio Gadiel Michael.
Nyangi alifanya kitendo hicho kisicho cha kiungwana kwa beki wa kushoto wa Yanga SC Gadiel Michael katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa Jumamosi iliyopita katika dimba la CCM Kirumba, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.




