Jumatatu , 17th Mar , 2014

Baada ya kikao kizito cha wang'amuzi wa vipaji jopo lafanya mchujo

Jopo wa wang’amuzi vipaji limetangaza majina ya wachezaji 36 waliopataikana katika mchakato wa maboresho ya Taifa Stars ulioshirikisha mechi za mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar

Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema jopo hilo liling’amua vipaji 143 katika mchakato, lakini waliochukuliwa kwa sasa ni hao 36 tu

Wachezaji hao 36 watapelekwa tukuyu mbeya kwa mafunzo kuanzia march 21 hadi 13 ambapo watachujwa na watakaobaki wataendelea na mafunzo hadi april 22 watakapounganishwa na wale wa kikosi cha sasa cha taifa stars.