Alhamisi , 2nd Jun , 2016

Timu ya Mbeya City inatarajiwa kufanya ziara ya michezo ya kirafiki nchini Malawi katikati ya mwezi huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.

Afisa Habari wa Mbeya City Dismas Ten amesema, mpaka sasa wamepata timu mbili ambazo watajipima nazo katika Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre kuanzia Juni 18.

Ten amesema, mchezo wa kwanza utakuwa ni dhidi ya vigogo wa soka nchini humo Big Bullets wakati Juni 21 itamenyana na Civo United.

Ten amesema, wameomba kucheza michezo mitatu hivyo timu nyingine watakayopambana nayo wataijua baada ya kufika nchini Malawi.