Jumapili , 27th Jun , 2021

Mwenyekiti wa Yanga Dkt. Mshindo Msolla ametangaza Baraza jipya la Wadhamini la klabu hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba

Msolla ametangaza Baraza hilo leo Juni 27, 2021 mbele ya wanachama kwenye Mkutano Mkuu wa klabu.

Katika Baraza hilo wamejumuishwa Mawaziri watatu wa Serikali ya Tanzania akiwemo Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.

1. George Mkuchika - Waziri Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum
2. Geofrey Mwambe - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji 
3. Abass Tarimba - Mbunge wa Kinondoni
4. Mama Fatma Karume - Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar
5. Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha na Mipango.