
Kikosi cha Bayern Munich kimeshinda mataji matano ndani ya kalenda ya mwaka 2020
Bao la ushindi la Bayern Munich lilifungwa na Joshua Kimmich dakika ya 82 baada ya timu hizo kuwa zimefungana mabao 2-2. Bayern waliongoza kwa mabao 2 yaliyofungwa na Correntin Tolisso na Thomas Mueller dakika ya 18 na 32, na Dortmund wakasawazishi mabao hayo kupitia kwa Julian Brandt dakika ya 39 na bao la Erling Braut Haaland dakika ya 55 kabla ya Joshua Kimmichkufunga bao la ushindi kwa Bayern.
Ushindi huo katika Dimba la Allianz Arena unaifanya Bayern kushinda taji la DFB Super Cup na sasa klabu hiyo inafikisha idadi ya mataji matono iliyoshinda ndani kya mwaka 2020, mataji mengi walioshinda mwaka huu ni ubingwa wa ligi kuu Ujerumani Bundesliga, klabu bingwa ulaya, ubingwa wa UEFA Super Cup na DFB Pokal.
The Bavarians wanaweza kuongeza taji la sita mwaka huu endapo kama watashinda taji la klabu bingwa ya Dunia michuano inayotarajiwa kufanyika Qatar ingawa bado tarehe ya kuanza haijathibitishwa.
Mafanikio haya ya Bayern yanamtengenezea mazingira mazuri kocha mkuu wa kikosi hicho Hans Flick kushinda tuzo ya kocha bora wa kiume ulaya lakini pia hata nahodaha Manuel Neuer na mshambuliaji Roberto Lewandowski ambao wanawania tuzo ya mchezaji bora wa kiume.
Kocha Flick anawania tuzo hiyo dhidi ya kocha Jurgen Klopp wa Liverpool na Julian Nagelsmann wa RB Leipzing katika tuzo hizo zinazotolewa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA.
Wakati Lewandowski na Manuel Neuer wanawania tuzo hiyo dhidi ya Kiungo wa Manchester City Kevin De Bruyne. Tuzo zitatolewa leo katika hafla ya upangaji makundi ya michuano ya klabu bingwa ulaya msimu wa 2020-21.