Katibu mkuu wa mchezo wa Baseball na Softball nchini Alferio Moris Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari juu ya ya mashindano ya Taifa ya michuano hiyo.
Jumla ya timu tisa kutoka mikoa ya Mbeya,Kilimanjaro,Ruvuma,Kisiwani Zanzibar,Mwanza pamoja na Dar es salaam zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo.
Katibu mkuu wa mchezo wa Baseball na Softball nchini Alferio Moris Nchimbi ameiambia East Africa Radio kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kutumika kusaka timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 itakayoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kusaka viwango vya ubora duniani mwezi februali mwakani nchini Africa Kusini.
Ameongeza kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano hayo ni Balozi wa Japan nchini ambaye atahudhulia kwenye mechi za mapema hii leo.