Ijumaa , 21st Jul , 2023

Timu ya Taifa ya kriketi chini ya umri wa miaka 19 imeendelea mazoezi yake ya kujiweka sawa katika viwanja wa Leaders , jijini Dar es salaam kwaajili ya mashindano ya Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika nchini kuanzia jumapili ya julai 22, 2023 mwaka huu katika viwanja vya Gymkhana

Meneja wa timu hiyo bwana Ally kimote amesema kuwa kikosi kinaendelea vyema huku kila mchezaji akiwa na shauku ya kufanya vyema katika mashindano hayo ili kupata nafasi ya Kwenda kucheza kombe la dunia nchini Sri Lanka .

‘’Kwa ujumla vijana wapo vizuri na wapo tayari kwaajili ya kufanya vizuri na kuitangaza nchini ya Tanzania katika mchezo huu wa kriketi ‘’ amesema Ally kimote

Mashindano hayo yatasharikisha nchini Zaidi sita ambazo ni Uganda , Kenya, Siera Lione , Namibia na mwenyeji Tanzania.