
Baada ya kutolewa katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika na timu ya Al Ahly ya Misri, mashabiki wa timu ya Dar es Salaam Young Africans wametaka kuwepo kwa utulivu katika timu hiyo na kuacha kutupiana lawama kutokana na matokeo hayo.
Baadhi ya mashabiki wa timu ya Yanga wamesema kuwa licha ya kutolewa kwenye michuano hiyo timu hiyo ilicheza soka kwa kiwango kikubwa, na kwamba hakuna sababu za mashabiki wala viongozi kutupiana lawama.