Mlinda Mlango wa zamani wa klabu ya Yanga Peter Manyika amesema, wasiwasi huwa inaanzia kwa mashabiki na kuhamia kwa viongozi na wasipokuwa makini wanawapa wachezaji ambao huwa wanakuwa hawana wasiwasi na mechi hiyo ya Simba na Yanga.
Manyika amesema, mara zote wachezaji huwa wanakuwa wameshajipanga kwa ajili ya kupambana kwani mechi ya Simba na Yanga huwa haina utabiri kwa madai kuwa mara nyingine timu mbovu ndiyo inashinda au zinatoka sare.
Manyika amesema, mechi hiyo ni ya kawaida sana tofauti na kukutana na timu nyingine na kwamba kinachoharibu mipango waliyojipangia ni wasiwasi wa viongozi na mashabiki.
Manyika amesema, kipindi alipokuwa akiidakia Klabu ya Yanga alikuwa anaona ni mechi za kawaida tofauti na wanapokutana na vilabu vingine.
Kwa upande mwingine Manyika amesema, vilabu vinavyowafukuza makocha baada ya timu kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea ndivyo vinavyochangia kushusha viwango vya timu.
Manyika amesema, vilabu vinakuwa na haraka na makocha bila kujua kuwa kocha anatakiwa kupewa muda ili kuwazoea wachezaji na kuwajua katika kila hali anapokuwa nao ili kuweza kuwaelewa mmoja mmoja na kuweza kupanga kikosi chake.
Manyika amesema, kocha anapowasili katika timu anakuta tayari wachezaji wameshaelewa programu ya kocha aliyeondoka huku uongozi ukitaka kocha mpya afanye vizuri huku akiwa muandaaji na aliyesajili mwingine.
Manyika amesema, viongozi wa vilabu wanajibana wao kwa kujificha kwa kosa la kumsingizia kocha ili waonekane wamefanya kazi bila kujua kuwa kufanya vibaya au vizuri kwa kocha inategemea na maandalizi.





