Jumatatu , 13th Apr , 2015

Marefa kutoka Nchini Msumbuji ndio watakaochezesha mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga na Etoile Du Sahel jumamosi wiki hii.

Yanga SC wataanza nyumbani kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano hiyo na baada ya kuzitoa BDF X1 ya Botswana na FC Platinum ya Zimbabwe ambapo Jumamosi hii watavaana na Etoile ya Tunisia.

Shirikisho la Soka Afrika CAF limewateua Marefa wa Msumbuji kuchezesha mechi hiyo Dar es salaam.
Marefa hao ni Samuel Chirindza atakayepuliza filimbi akisaidiwa na wapeperusha vibendera Arsenio Chadreque Marengula na Celio De Jesus Mugabe.