Alhamisi , 8th Feb , 2018

Afisa habari wa Klabu ya Simba Haji Manara amewaonya mashabiki wa wekundu wa Msimbazi kuacha kuwazomea mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga katika mchezo wa kimataifa dhidi ya St. Louis siku ya Jumamosi.

Afisa habari wa Klabu ya Simba Haji Manara

Manara ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Kariakoo Msimbazi, jijini Dar es Salaam na kuwaomba mashabiki wa soka nchini kuuziunga mkono timu zao za nyumbani Simba na Yanga kama timu zinazo wakilisha nchi na kuacha tamaduni za kuzomeana  na kuvunjana moyo

"Natoa wito kwa washabiki wa Simba watakaoenda uwanjani kwenye mechi ya Yanga Jumamosi wasiizomee,tuzomeane kwenye ligi ya nyumbani. Sisi sote ni watanzania na tunawakilisha nchi", amesema Manara.

Kwa upande mwingine, timu ya Simba inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumapili (Februari 11, 2018) kuvaana na Gendemerie Nationale katika mchezo wao wa kimataifa huku  Rais wa awamu ya pili Al Haji Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo