Jumatatu , 8th Mei , 2017

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, limeungana na waombolezaji wa msiba jijini Arusha na kutoa salamu za rambi rambi na kusema kuwa kwa upande wao ajali hiyo imewapoteza vijana ambao ni ndoto ya TFF yenye lengo la kuinua vipaji mashuleni.

Salamu hizo za rambirambi zimetolewa na rais wa (TFF), Jamal Malinzi ambapo ameungana na viongozi mbalimbali kuomboleza msiba huo na kutoa rambirambi ya Sh. 500,000 kwa walengwa waliopoteza watoto katika ajali hiyo.

“Mtazamo wetu kwa sasa ni kuendeleza soka la vijana, tena hasa wale walioko mashuleni hivyo vijana wale ni sehemu ya kutimiza ndoto za TFF katika mpira wa miguu hapo baadaye, tunakubali haya yote kwa kuwa ni ya Mwenyezi Mungu ndiye anayejua siri,” amesema Malinzi.

Hata hivyo, Malinzi amewataka wanafamilia wote wa mpira wa miguu kuwaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi.