Jumanne , 22nd Sep , 2015

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amefunga kozi ya makocha ya leseni C inayotolewa na CAF, iliyowashirikisha makocha 31 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amefunga kozi ya makocha ya leseni C inayotolewa na CAF, iliyowashirikisha makocha 31 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akifungua kozi hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Soka mkoa wa Dar es salaam (DRFA), Malinzi amewaomba washiriki wa kozi hiyo kwenda kutumuia ujuzi walioupata kwa kufundisha timu na vituo vya vijana vilivyopo sehemu mbalimbali.

Malinzi amewaomba makocha hao kwenda kufundisha mpira na sio kwenda kuviweka vyeti hivyo makabatini, ambapo TFF inaandaa mpango maalum kuendeleza vijana kwa ajili ya ushiriki wa vijana kwenye fainali za mataifa Afrika kwa vijaa wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2017 nchini Madagascar, mwaka 2019 Tanzania na baadaye tuweze kushiriki fainali za Olimpiki mwama 2010 Tokyo nchini Japan.

Aidha Malinzi amewataka walimu walioshiriki kozi hiyo akiwamo kocha msaidizi wa Simba Suleiman Matola, kushinikiza viongozi wa timu zao kupeleka timu za wanawake kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa ya wanawake inayotarajiwa kuanza baadaye mwaka huu, ambapo Matola alisema Simba Queens ipo tayari kucheza ligi ya wanawake.