Ijumaa , 1st Mei , 2015

Wakufunzi wa ukocha wa mpira wa miguu hapa nchini wametakiwa kufundisha ili kuwa na uzoefu ili anapotoa mafunzo kwa wengine aweze kufundisha kutokana na uwezo wake binafsi.

Akizungumza na East Africa Radio, mkufunzi wa makocha wakufunzi wa shirikisho la soka nchini TFF, Sunday Kayuni, amesema, wakufunzi wenye uwezo wa kusaidia wanatakiwa kuandaliwa mapema lakini anatakiwa kuwa na uwezo wa kufundisha kwani ngazi ya ukufunzi ni kubwa, hivyo ni lazima uwe na uwezo wa kutoa elimu kwa wengine.

Kayuni amesema, uzoefu wa kufundisha na kuwa mkufunzi ni vitu viwili vinavyoendana hivyo unaposimama mbele ya wale unaowafundisha wanatakiwa kuelewa kile wanachofundishwa.