
Kushoto ni bondia Maxim Dadashev na kulia ni bondia Hugo Santillan.
Wiki hii imekuwa si nzuri kwa mchezo huo kutokana na mabondia wawili kupoteza maisha baada ya kuumia wakiwa ulingoni.
Bondia Maxim Dadashev mwenye miaka 28, raia wa Urusi amefariki Jumanne Julai 23, 2019, ikiwa ni siku 4 zimepita baada ya kutoka ulingoni alikokuwa akipigana na Subriel Matias kwenye pambano la (IBF) Junior welterweight Ijumaa Julai 19 huko Maryland.
Kuna video zinaonesha jinsi mkufunzi wa Dadashev akimsisitiza bondia huyo wasitishe pambano kwani alikuwa na hali mbaya ikiwemo mwili kuchemka kupita kiasi.
#VIDEO Bondia Maxim Dadashev (28) akiulizwa na mkufunzi wake wasitishe pambano kutokana na yeye kuchemka sana. Baada ya siku 4 Maxim ambaye ni raia wa Urusi alifariki dunia kwa majereha kwenye ubongo. Pambano hilo lilikuwa la (IBF) Junior welterweight, lilipigwa huko Maryland. pic.twitter.com/D4zOZvkh9P
— East Africa Radio (@earadiofm) July 26, 2019
Imeelezwa kuwa Dadashev alikuwa na tatizo kwenye ubongo lililotokana na kupigwa ngumi katika mapambano yake mbalimbali yaliyopita pamoja na hilo la Ijumaa.
Bondia mwingine ambaye amefariki wiki hii ni Hugo Santillan mwenye miaka 23 raia wa Argentina, ambaye amefariki baada ya kupigwa na kupoteza fahamu katika pambano dhidi ya Eduardo Abreu wa Uruguay.
Santillan alikimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji wa ubongo na kinga ya mwili lakini amefariki siku 5 baada ya pambano hilo.
#FAHAMU Bondia Hugo Santillan (23) wa Argentina, amefariki baada ya kupigwa na kupoteza fahamu katika pambano dhidi ya Eduardo Abreu wa Uruguay. Santillan alikimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji wa ubongo na kinga ya mwili lakini amefariki siku 5 baada ya pambano hilo. pic.twitter.com/sNWDbwSGNY
— East Africa TV (@eastafricatv) July 26, 2019
Santillan na Eduardo Javier walipigana Jumatano usiku huko Buenos Aires Argentina, kwenye pambano la Super lightweight.