Mshambuliaji wa Yanga SC, Malimi Busungu
Busungu amesema, Mabeki wote ni wakawaida na wanapitika, kikubwa ni mipango tu.
Akizungumzia kuelekea mpambano wao wa Jumamosi dhidi ya mahasimu wa jadi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Busungu amesema, kikubwa ni timu kushinda na hawaangalii nani kafunga.
Busungu amesema, kila timu ina mapungufu yake na kwa upande wao pia kuna mapungufu lakini inategemea nani atatumia vizuri makosa ya mwenzake, ila wao wamejipanga vizuri kwa ajili ya kushinda mechi hiyo.
Busungu alisajiliwa na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara akitokea Mgambo ambapo katika mzunguko wa kwanza aliipatia timu yake bao moja kati ya mawili walipowapiga watani wao wa jadi 2-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.




