
Katika taarifa yake, Kocha mkuu wa Timu hiyo Stewart Hall amesema, wapo katika mapumziko ya siku nne ambapo Ijumaa watakutana na kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa ngao ya jamii pamoja na Ligi kuu Soka Tanzania Bara.
Hall amesema, Yanga anaifahamu vizuri kwani wameshaifunga katika Kagame japo hajaridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake hivyo presha kubwa ipo katika timu nyingine za chini ambazo zinadharauriwa kwa kwa kushindwa kuleta ushindani.