Jumanne , 25th Oct , 2016

Meneja wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp amesema timu yake bado haijafikia asilimia 100 msimu huu, ingawa timu hiyo haijapoteza hata mechi moja katika michezo tisa iliyopita.

Liverpool katika mazoezi

Liverpool watakuwa wenyeji wa Tottenham hii leo Jumanne katika raundi ya nne ya Kombe la Ligi wakiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo mwa EPL, na wakiwa sawa na pointi na klabu ya Manchester City, ambayo ndiyo inaongoza ligi hiyo na timu ya Arsenal ambayo iko katika nafasi ya pili.

Inatarajiwa kwamba bosi wa Tottenham Mauricio Pochettino atapumzisha mlinda mlango Hugo Lloris, na hii inamaanisha kuwa Michel Vorm atachukua nafasi ya Lloris kuanzia mwanzoni mwa mchezo huo.