Nembo ya bodi ya ligi Tanzania.
Jumamosi katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, Maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha Maafande wa Mgambo Shooting, Toto Africans watawakaribisha Tanzania Prisosns uwanja wa CCM Kirumba, huku Stand United wakicheza dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Uwanja wa Tafa jijini Dar es salaam, Simba SC watawakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar saa 10 jioni, Mbeya City watakua wenyeji wa Mwadui FC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Coastal Union dhidi ya Majimaji uwanja wa Mkwakwani, huku mchezo kati ya Azam FC dhidi ya African Sports ukianza saa 1 usiku.
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa mchezo mmoja katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Young African watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara.

