
Uwanja wa Taifa mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakutana na Mbeya City huku uwanja wa Kambarage Mwadui FC akiwakaribisha wekundu wa Msimbazi Simba SC na Mtibwa Sugar atakuwa mwenyeji wa Mgambo Shooting.
Mtwara Ndanda atawakaribisha JKT Ruvu Songea atawakaribisha wajelajela Tanzania Prisons huku Tanga Coastal Union Stand Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Baraka Kizuguto amesema, michuano hiyo itamalizika Jumapili katika mzunguko huo wa 12 kwa michezo miwili kupigwa ambapo CCM Kirumba Toto African akiwakaribisha African Sports. huku Azam FC wakiwakaribisha Kagera Sugar.
Kizuguto amesema, Desemba 30 Azam FC atacheza mchezo wake wa kiporo kwa kuikaribisha Mtibwa Sugar huku Januari Mosi mwakani Ndanda FC ataikaribisha Simba ili timu zote ziwe zimecheza michezo sawa ambapo ligi itaendelea tena Januari 16 ili kuweza kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.