Jumanne , 18th Nov , 2014

Michuano ya Ligi Daraja la pili Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii katika viwanja mbalimbali hapa nchini kwa kushirikisha timu 24 makundi manne.

Akizungumza jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF,Boniface Wambura amesema mechi hizo zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini huku kila timu katika kundi itapanda na kucheza Ligi Daraja la kwanza msimu ujao.

Wambura amesema kila timu inatakiwa kufuata sheria zote za soka nchini ili kuweza kuepukana na vurugu zinazotokea Uwanjani ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kuvurugika kwa mechi.