Lee Carsley anatarajiwa kutangazwa kuwa kaimu kocha mkuu timu ya taifa ya England
Inaripotiwa kuwa Kocha huyo ataanza kibarua mwezi ujao kuwaongoza Three Lions katika michuano ya Uefa Nations League huku FA ya taifa hilo ikiendelea na mchakato wa kutafuta kocha wa kudumu ambaye atachukua nafasi ya Gareth Southgate ambaye alijiuzulu baada ya fainali za michuano ya EURO 2024.
Makocha wanaohusishwa na kibarua cha kuinoa England ni Eddie Howe, Graham Potter, Mauricio Pochettino na Kieran McKenna.