Jumanne , 18th Aug , 2020

Aliyewahi kuwa Kocha wa Klabu ya Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger amekusudia kurejea tena katika majukumu ya kufundisha soka baada ya kutuma maombi rasmi kwenye chama cha soka cha Uholanzi.

Enzi kocha Arsene Wenger (Kulia) na aliyekua nahodha katika klabu ya Arsenal, Thiery Henry (Kushoto) wakifurahia kazi nzuri .

 

Taarifa kutoka nchini Hispania zimebainisha kuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, Ronald Koeman atatangazwa kuwa ndiye mwalmu mpya wa Barcelona ambayo imemfuta kazi Quique Setien.

Wenger amekaa miaka miwili bila kufundisha soka tangu alipotangaza kuondoka Arsenal mwaka 2018 .

Raia huyo wa Ufaransa anataka kurejea katika soka tena na kwa sasa anaangalia zaidi timu za Taifa tofauti na muda mwingi aliyeutumia kufundisha ngazi ya klabu.

KAZI KUBWA YA WENGER.
Endapo Wenger atapata nafasi hiyo atakuwa na jukumu kubwa la kuifanya Uholanzi ifuzu kwenye kombe la dunia la mwaka 2022 pamoja na michuano mbalimbali ya Ulaya kwa sababu Taifa hili kubwa kisoka lilishindwa kufuzu kwenye kombe la dunia la 2018 Russia

JE UHOLANZI INAMHITAJI WENGER?KWA NINI?

Kwa mujibu wa wachambuzi wa mpira wa miguu, wengi wanaamini kuwa, Uholanzi watakua wamefanya chaguo sahihi kwa kuwa Taifa lao limebarikiwa vipaji vya hali ya juu.

Lakini vipaji hivyo vinahitaji mwalimu mwenye uwezo wa kuwafanya wajiamini na kuwatambulisha kuwa wakubwa kwenye ramani ya soka.

Wenger alithibitisha hilo kupitia vijana wadogo kama Marc Overmars, Denis Bergkamp,Nicolas Anelka, Patrick Vieira, Fredrick Ljunmberg, Thiery Henry, Sol Campbell, Ashley Cole , Robert Pires, Silyvain Wiltord, Lauren Etame Mayer wote walipitia mikononi mwake.

Wengine waliokua mastaa baada ya kupita kwenye mikono ya Wenger ni pamoja na Emmanuel Adebayor, Alexander Song, Gervinho,Cesc Fabrigas, Samir Nasri , Gael Clichy bila kusahau mwamba wa EPL, Robin Van Persie.

Uholanzi ina vijana ambao wana vipaji lakini havijafanikiwa kutikisa dunia bila ya sababu za msingi mfano Memphis Depay, Gigi Wijnaldum, Frank De Jong, Matthis De Ligt na wengi ambao wanahitaji kocha wa aina ya Wenger.

Ikizingatiwa Wenger ni muumini wa soka la vijana, na Uholanzi ambayo ina vilabu vinavyozalisha wachezaji wengi ikiwemo Ajax, ni moja ya sababu ambayo upo uwezekano mkubwa wakafanikiwa kuteka soka la dunia zaidi ya ilivyo hivi sasa.