Alhamisi , 19th Jan , 2023

Kuelekea mchezo wa kirafiki kati ya Saudi All Stars dhidi ya PSG hi leo, Baadhi ya mashabiki nchini Saudi Arabia wamelipa dola milioni 2.6, sawa na zaidi ya Tsh billioni 6 kwa ajili ya tiketi za 'V.I.P' kuwaona Ronaldo na Messi huku wao wakiwa kama wageni waalikwa.

Messi na Ronaldo

Tiketi hii itampa muhusika fursa ya kuhudhuria sherehe ya ufunguzi kabla ya mchezo huo, na pia kukutana na wachezaji wote maarufu kama vile Ronaldo, Messi, Neymar Jr, Kylian Mbappé na wengine wengi wa PSG.

Pia watapata fursa ya kusalimiana nao na kupiga nao picha za kumbukumbu wakiwa vyumba vya kubadilisha nguo, pamoja na wakati wa sherehe za ufunguzi. 

Mchezo huo wa kihistori wa kirafiki unatarajia kupigwa majira ya saa 2:00 Usiku wa leo Alhamis Januari 19, 2023 kwa saa za Afrika Mashariki.