Mfungaji bora wa mashindano hayo Omary Marungu akifunga goli la kwanza
Mtibwa wametwaa ubingwa huu kwa mashindano ya vijana kwa timu za ligi kuu , kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo mwaka jana kwa kuwafunga Azam U-20 kwa penati 4-2 baada ya kwenda suluhu kwa dakika 120
Timu hiyo ya vijana imekuwa inafanya vizuri miaka ya karibuni,tofauti sana na timu yao ya wakubwa ambayo kwa mara ya mwisho ilitwaa ubingwa miaka 21 iliyopita,misimu miwili hii imekuwa katika hatari kubwa ya kukaribia kuporomoka daraja.
Maswali ni mengi wapi Mtibwa wanafanikiwa , kuna siri gani iliyofichika ndani yake? ni kweli timu za vilabu vya Simba Yanga na Azam zimeshindwa kupata muarobani wa kupambana nayo, kuna uwekezaji gani tofauti kwenye timu za vijana hadi kupata mafanikio hadi kuwafanya watwae ubingwa mfululizo.
Timu hiyo ya Mtibwa U-20 pia ilijizolea tuzo nyingi za mashindano hayo kama kocha bora iliyokwenda kwa Awadh Juma, Omary Marungu akipata ya mfungaji bora, Jojo Mkele alitajwa kuwa kiungo bora wa mashindano pamoja na mchezaji bora wa ujumla.