
Kocha Unai Emery mwenye mafanikio katika Europa league
Unai aliongoza timu yake ya Villarreal kuibuka mabingwa baada ya kuwafunga Manchester United kwa mikwaju ya penati 11 kwa 10 baada ya kwenda sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo ma ule wa nyongeza.
Wachezaji wa Villarreal wakimpongeza kocha wao Unai Emery
Villarreal walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 35 kwa goli lililofungwa na Gerrard Moreno, huku Manchester United wakisawazisha kupitia mkongwe Edinson Cavani ktika dakika ya 55 ya mchezo akimalizia mpira uliyotemwa na golikipa Rulli ambaye alikuwa shujaa wa mchezo baada ya kuokoa penalti ya mwisho iliyopigwa na David De Gea.
Wachezaji wa Villarreal wakishangilia ubingwa wao
Unai amekuwa na rekodi nzuri kwenye michuano hii akiwa amecheza fainali 5 na kuibuka mshindi mara 4 kwa amefanya hiyo akiwa na timu ya Sevilla (2014,2015,2016) na Mwaka 2020-2021 akiwa na Villarreal, mwaka 2019 akiwa Arsenal alipoteza fainali yake kwa kufungwa na Chelsea.