Ijumaa , 27th Mar , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa Kriketi inatarajia kushuka Dimbani kucheza na Uganda katika mchezo wa Ufunguzi katika mashindano ya Afrika Ligi ya Daraja la kwanza yanayotarajiwa kufanyika Mwishoni mwa mwa wiki hii Nchini Afrika Kusini.

Katika Taarifa yake, Nahodha wa Kikosi cha Tanzania Hamis Abdallah amesema, Uganda sio timu ngeni kwao hivyo wamejiandaa vyema kukabiliana nao.

Nahodha huyo mwenye rekodi ya kucheza nchini Uingereza, katika Klabu ya Watford Town ameendelea kuwa Nahodha wa Tanzania zaidi ya miaka 10 hivyo ana uzoefu mkubwa sana.

Nchi nyingine zinazotarajiwa kushiriki katika michuano hiyo ni Kenya, Namibia, Botswana na Ghana.