Jumapili , 7th Dec , 2014

Mashindano ya Afrika ya Kriket ya wasichana chini ya miaka 19 yameanza leo uwanja wa Gymkhana jijini
Dar es salaam, kwa kushirikisha timu kutoka nchi Sita Barani Afrika.

Akizungumza na East Afrika Radio, Meneja wa michuano hiyo, Kazzim Nassa amesema michuano hiyo yenye ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji kushika nafasi za juu inashirikisha nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Msumbiji, Botswana na wenyeji Tanzania.

Kazzim amesema baada ya kumaliza mashindano hayo, Desemba 12 mwaka huu timu ya Taifa itaelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kijiandaa na mashindano ya kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Duni inayotarajiwa kuanza Desemba 14 mwaka huu.

Kazzim amesema katika michuano hiyo kuna baadhi ya wachezaji walio katika timu ya wasichana ya chini ya miaka 19 ambayo itajiunga na timu ya Taifa baada kumaliza michuano hiyo inayotarajiwa kumalizika Desemba Tisa mwaka huu.