Mabondia Francis Miyeyusho (Kushoto) na Francis Cheka (Kulia) wakiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Katikati) nje ya ukumbi wa Bunge 2013
Maandalizi ya mipambano miwili ya kimataifa itakayowahusisha mabondia wawili kutoka Tanzania, Francis Cheka na Francis Miyeyusho na mabondia kutoka nje ya nchi yamekamilika,
Kwa mujibu wa mratibu wa mapambano hayo ya kimataifa ya ngumi za kulipwa Musa Kova amesema kuwa kwa asilimia kubwa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni ujio wa wapinzani hao ambapo mpinzani wa Frncis Cheka anataka nchini Iran na mpinzania wa Francis Miyeyusho yeye akitokea nchini Ufilipino.
Naye mratibu msaidizi wa mpambano huo ambaye awali aliandaa mpambano wa dunia kati ya Cheka na Phill Williums toka Marekani promota Jay Msangi amesema watanzania watarajie burudani ya aina yake siku hiyo kutokana na ubora na uwezo wa mabondia watakaokutana siku hiyo na akamtaadharisha Cheka kuwa asitegemee mteremko kutoka kwa bondia huyo wa Irani kwani ana historia nzuri katika michezo aliyokwisha cheza