Jumanne , 29th Jun , 2021

Mnamo Juni 29, 1958, gwiji wa soka Edson Arantes do Nascimento (Pelé) aliiongoza timu ya Taifa ya Brazil kushinda Kombe la Dunia la kwanza kwa kuwatungua wenyeji Sweden mabao 5-2. 

Picha ya Edson Arantes do Nascimento

Brazil iliingia kwenye mashindano hayo kama kipenzi cha watu wengi, haikukatisha tama bali iliwafurahisha wapenzi wa soka ulimwenguni kote kutokana na mchezo wao wa kupendeza, ambao mara nyingi uliitwa "mchezo mzuri".