
Kocha wa Simba Patrick Aussems
Aussems ameyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari uliohusisha makocha wa timu zote mbili, ambapo mbali na ushindi amesema kikosi chake kipo salama.
“Tupo tayari na tunajua tunataka kushinda, tutafanya kila kitu kufanikisha hilo na wachezaji wanajua hilo. Tunatakiwa kuwa makini, tunajua tunakutana na timu nzuri na utakuwa mchezo mgumu lakini tunajiamini'', Patrick Aussems.
Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote katika mchezo huo kutokana na suluhu iliyopata ugenini wiki mbili zilizopita. Mchezo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 10:00 jioni.