
George Leekens
Leeken raia wa Ubelgiji amesema amemua kwa moyo mkunjufu kuacha nafasi hiyo, bila ya kushinikizwa.
"Kwa nia njema kabisa nimeamua kuacha ingawa nafanya hivi kwa uchungu moyoni, na naitakia kila kheri timu ifanye vyema kimataifa". Aliandika kocha huyo kwenye tovuti ya AFF.
Alikabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo mwezi Oktoba mwaka jana (2016) akitokea klabu ya Lokeren na Ubelgiji ambako alikwenda baada ya kuachana na timu ya Taifa ya Tunisia aliyoinoa kwa miaka miwili yaani 2014 na 2015.
Algeria iliyokuwa inapigiwa upatu kutwaa taji hilo, imemaliza nafasi ya tatu katika kundi B, ikifungwa mechi moja dhidi ya Tunisia, na kutoka sare na Zimbabwe na Senegal.