Kocha Nasra amesema, Twiga Stars ya miaka miwili nyuma sio ya sasa kwani kwa sasa wanawachezaji wadogo ambao wananguvu na ni vipaji vipya ambavyo vitaweza kuiweka timu katika nafasi nzuri.
Nasra amesema, kikosi chake ameanza kukiboresha kwa kuongeza wachezaji wawili kutoka visiwani Zanzibar ambao ni Nasreen Mohamed na Aziza Mtumwa ambao amewapata katika mchujo wa kutafuta wachezaji wenye vipaji ambao wataweza kujiunga na kikosi cha Twiga ambao walijitokeza wachezaji wachezaji 22 na akapata vipaji vya wachezaji wawili.
Nasra amesema, viongozi na wadau mbalimbali wa soka wanatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kuweza kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri zaidi katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.






