Jumanne , 19th Sep , 2023

Kocha wa Singida Fountain Gate FC, Ernest Middendrop ameondoka kwenye klabu hiyo na kuelekea nchini kwao Afrika Kusini na kuacha sintofahamu klabuni hapo huku sababu ikielezwa ni kutoelewana na Uongozi wa klabu hiyo.

Kocha wa Singida Fountain Gate FC, Ernest Middendrop

Akizungumza sintofahamu hiyo, Afisa Habari wa Singida Fountain Gate FC, Hussein Massanza amesema Kocha huyo ameondoka Jumatatu ya Jana Septemba 18, 2023 na nafasi yake imeshikiliwa kwa muda na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo Ramadhan Nsanzurwimo.

“Bado ana mkabata na klabu yetu hivyo amekwenda Afrika kusini kushughulikia mambo yake binafsi na yakikamilika atarejea katika kikosi hicho kwani sisi hatujamfukuza na wala hatuna mazungumzo ya kuvunja mkabata kwahiyo tunatambua uzoefu wake “amesema Masanza.

Kwa upande mwingine Masanza amesema kikosi chao kimerejea mazoezi leo Jumanne ya Agosti 19, 2023 kujiandaa na mchezo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania dhidi ya Azam Fc utaopigwa Alhamis ya Agosti 21, mwaka huu kwenye dimba la Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo Ernst Middendrop alijiunga na Singida Fountain Gate FC wiki mbili zilizopita na ameisimamia klabu hiyo kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Future FC ya Misri kwenye mchezo wa kwanza kuwania kufuzu makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.