
Yanga Vs MC Alger, Dar es Salaam
MC Alger inaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Stade du 5 Juillet 1962, jijini Algiers, Jumamosi hii, huku kocha wao akiamini wanavuka kwenda hatua ya mtoano.
"Nadhani tungefunga goli Tanzania, lakini tulikosa ufanisi mbele ya goli.... Kuna baadhi ya mambo hayakwenda vizuri, na hatuachi kufanya makosa yaliyojirudia." alisema Mouassa akiongea na Le Buteur.
Pamoja na kupoteza mchezo huo, Mouassa amesema hatafanya mabadiliko kwenye kikosi kilichopoteza mchezo wa Dar es Salaam.
"Tunajiandaa na mechi hii kikawaida, tofauti na mechi ya kwanza ambayo hatukujua lolote kuhusu hii timu ya Yanga," aliendelea Mouassa. "Sasa najua nguvu na udhaifu wa wapinzani wetu, na sitaki kujiingiza katika hili, kwa sababu hata kama kuna namna ya kufuzu, lakini sitaweka wazi,"
MC Alger walijitahidi kuibana Yanga kwenye mchezo uliopigwa Dar es Salaam, lakini walitereza kunako katika dakika ya 66, pale Mzimbabwe Thabani Kamusoko, alipowafungia mabingwa hao wa Tanzania bao pekee
Kamel Mouassa kocha wa MC Alger