Ijumaa , 25th Dec , 2015

Kocha Mkuu wa Majimaji, Mika Lonnstrom, amefungashiwa kila kilicho chake rasmi na kisha mikoba yake ipo mbioni kuchukuliwa na kocha msaidizi wa timu hiyo, Hassan Banyai.

Mika aliondoka nchini Novemba 20, mwaka huu ambapo uongozi wa klabu hiyo umedai kuwa kuondoka kwake kumetokana na kibali chake cha kuishi, kuisha muda wake.

Chanzo kutoka Majimaji kimefunguka kuwa kocha huyo ameondoka nchini kutokana na kushindwa kuelewana na uongozi wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na malipo ya mshahara.