Klabu ya KMC
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao kwa dakika tisini zilikamilika kwa sare ya bao moja na kulazimika kupiga matuta ambayo KMC haikupata hata moja huku Kagera Sugar ikipata matuta mawili, kocha huyo amesema kwa kiogozi wa timu anayefahamu mpira matokeo hayo ni jambo la kawaida.
Kwa upande wake kocha wa Kagera Sugar, Meck Mixime amewashukuru wachezaji wake kwa kuiwezesha timu hiyo kusonga mbele katika michuano na kuwa sasa wanajiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prison utakaopigwa Jumamosi.
Mlinda mlango wa Kagera Sugar, Ramadhan Charamanda aliyefanya kazi kubwa ya kuivusha timu yake kwenda robo fainali kwa kupangua penati mbili, amesema kuwa alijitahidi kufuata maelekezo ya mwalimu wake.
Kagera Sugar imeungana na timu za Simba SC, Yanga SC, Kagera Sugar, Alliance FC, Azam FC, Namungo FC, Sahare All Stars na Ndanda FC katika hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo.

